Zaidi ya vijana 100 wajitokeza kwenye zoezi la TISA mapema hii leo katika uwanja wa Green eneo la Magutu.
Zoezi hilo lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la SambaSports Youth Agenda kupitia mradi wake wa Shared Futures uliwavutia vijana wengi kutoka wadi ya Ukunda gatuzi la Kwale.
Akizungumza katika hafla hiyo Pastor Shadrack Maithia wa Glory Evangelism Ukunda aliwasihi vijana hao kua na heshima kwani ndio njia pekee itakayowawezesha kufikia malengo yao na kwamba kuna laini wakiifata watakua wanavyotoka na laini nyengine wakiifata hawatokua vile wanavyotaka.
Pia aliwasisitiza kufahamu kwamba wote wameumbwa na mungu na hakuna alobaguliwa hivyo basi wanafaa kushirikiana,kupendana na
Kuheshimiana pasi na tofauti zao za kidini.
Sheikh Amani Mwachirumu aliwapa vijana hao mifano iliyohai ya wachezaji mahari kama vile Origi na Ronaldo ambao hawatumii mihadarati tofauti na wachezaji wengine ili kulinda na kuzidi kukuza vipaji vyao.
Mwachirumu aliwasifu vijana hao kwa kuonyesha nidhamu na kuwaelezea ya kwamba nidhamu ndio ufunguo wa mambo mengi katika maisha yao na kwamba mtoto mkaidi hafaidi mpaka siku ya iddi.
Wakati huohuo kijana mwenye ulemavu wa kutembea anaefahamika kama Hamisi Bakari alivutiwa na kazi ya shirika la SambaSports na akawahimiza vijana hao kutilia manani nafasi waliopewa kushiriki kwenye warsha hizo ili kuweza kukuza vipaji vyao kwani yeye anatamani apate nafasi hiyo lakini muumba hakosolewi.
Michezo mbalimbali kama vile kandanda, Tug of war, filling the bottle na Paper race ilishirikishwa kama njia moja wapo ya kupitisha ujumbe wa zoezi hilo.
Vijana hao walizawadiwa zawadi kemkem zikiwemo mswaki,dawa ya mswaki,vichana, sabuni ya kuoga,mafuta ya kujipaka na suruale za ndani na mshindi wa siku kujinyakulia kombe zuri mno.Pia walipewa maziwa na mkate ili kuweza kutuliza tumbo. Shared Futures ni mradi unaopania kuieleza jamii kwamba tofauti zetu ni baraka na sio laana.
Mwadishi: Nrasiku Mwadama