Watoto ni kundi kubwa linalotumiwa kuleta tofauti za kidini katika jamii na hivyo basi wanahitaji muongozo bora ili kuiga misingi bora ya maisha na kukataa kutumika vibaya.
SambaSports Youth Agenda kupitia mradi wake wa Shared Future imeunda miundo misingi kupitia zoezi la TISA kutimiza shughuli hiyo.
Zoezi hilo linalodhaminiwa na shirika la Kerk in Actie limeanza rasmi mapema hii leo katika uwanja wa Duza na Kombani Force mtwalia ambapo linatarajiwa kuwafikia vijana 400 kutoka kaunti za Kwale na Mombasa.
Michezo mbalimbali kama vile kandanda, Tag of war,Paper Palk na mpira wa wavu wa miguu ilishirikishwa kama njia moja wapo ya kupitisha ujumbe wa zoezi hilo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Ustadh Amani Mwachirumu aliwafundisha vijana hao kuhusu gonjwa la corona ikiwemo athari zake na vipi mtu anaweza kujikinga kutokana na janga hilo na pia kuhusiana na maswali ya elimu na vipi wanaweza kua watoto bora.
Pia aliwasisitiza vijana hao kua wao ni ndugu moja na hivyo basi wasitenganishwe na misingi ya dini zao.
Wakati huohuo pastor Evans Onyango aliwahimiza vijana hao kua dini ni njia moja
wapo ya kumjua na kumtambua mungu. Pia aliwasisitiza kuvumiliana na kukubaliana licha ya tofauti zao na kufanya kazi pamoja au kushirikiana licha ya misingi yao ya kidini.
Onyango aliwahimiza vijana hao kua kielelezo bora katika jamii na wakatae kutumika vibaya. Alilipongeza shirika la SambaSports kwa kuandaa tamasha kama hizi na kuomba zifanyike mara kwa mara.
Vijana wote walioshiriki kutoka madrassahs, sunday schools na kutoka mtaani walipata zawadi za kila aina zikiwemo miswaki, dawa za mswaki, sabuni za kuoga na suruali za ndani.Timu iliobuka mshindi kutoka pande zote mbili ilijinyakulia kombe maridadi sana.
Pia vijana hao waliweza kupewa maziwa na mkate ambapo walifurahia sana na kuomba watembelewe kila mara.
Shared Future ni mradi unaopania kuieleza jamii kwamba tofauti zetu ni baraka na sio laana.
Mwandishi: Nrasiku Mwadama